Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Baba Askofu Dkt Fredrick Shoo akitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Isalia Elinewinga wakati wa shughuli ya mazishi iliyofanyika kijiji cha Losaa Masama Magharibi wilayani Hai.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Isalia Elinewinga.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa Waziri wa Elimu wa zamani ,Isalia Elinewinga aliyezikwa nyumbani kwake kijiji cha Losaa wilaya ya Hai.
Baadhi ya waombolezaji walifika kwenye msiba huo.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ,Prof Joyce Ndalichako akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala wakiwa katika mazishi ya Marehemu Isalia Elinewinga.nyuma yao ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka.
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe pamoja na mkewe Dk. Lilian Mtei wakiwa katika mazishi ya marehemu Elinewinga.
Familia ya Marehemu Elinewinga wakiwa wenye huzuni kando ya jeneza lenye mwili wa mpendwa Baba yao mzee Isalia Elinewinga.
Baadhi ya waombolezaji walifika katika mazishi hayo.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Elinewinga likiwa limebebwa tayari kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Jeneza likishushwa katika kaburi .
Mkuu wa KKKT ,Dkt Fredick Shoo akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Isalia Elinewinga.
Jeneza likishushwa kaburini.
Asko Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini,Erasto Kweka akiweka mchanga katika kaburi.
Mmoja wa wajukuu wa Marehemu ,Isalia Elinawinga akiwa ameshikilia picha kubwa ya mpendwa babu yake .
Waziri Ndalichako akiwa amekaa jirani na mjane wa Marehemu Isalia Elinewinga wakifuatilia uwekaji wa mwili wa marehemu katika kaburi.
Familia ya Marehemu Isalia Elinawinga wakionekana wenye huzuni wakati jeneza lenye mwili wa baba yao likiwekwa kaburini.
Mkuu wa KKKT ,Dkt Fredrick Shoo na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Isalia Elinewinga.
Askofu Mstaafu wa KKKT,dayosisi ya Kaskazini Erasto Kweka akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Elinewinga.
Mjane wa Marehemu ,Isalia Elinewinga akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mumewe.
Mtoto mkubwa wa marehemu Elinewinga,David Elinewinga akisaidiana na mkewe kuweka shada la maua katika kaburi la baba yao.
Mtoto wa marehemu Elinewinga,Adam Elinewinga akiwa na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi.
Wajukuu wa matrehemu wakiweka shada la maua katika kaburi.
Makamau mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Philip Mangula akiweka shada la Maua katika kaburi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiweka shada la maua katika kaburi.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na mkewe Dkt Lilian Mtei wakiweka shada la maua katika kaburi.
Mbunge wa Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy akiweka shada la maua katika kaburi.
Prof Ndalichako akizungumza jambo na mjane wa marehemu Elinewinga wakati wa mazishi .
Mkuu wa KKKT ,Dkt Fredrick Shoo akimuelezea marehemu Elinewinga wakati wa shughuli ya mazishi.
Baadhi ya waombolezaji.
Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini ,Erasto Kweka akizungumza namna alivyomfhamu marehemu.
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema akiwa mmoja wa waombolezaji waliofika katika mazishi hayo.
Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi akitoa salamu za serikali katika mazishi ya marehemu Elinewinga.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Philip Mangula akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akimuelezea marehemu namna alivyo mfahamu.
Mbunge wa jimbo la Hai ,Freeman Mbowe akizungumza katika mazishi ya marehemu alinewinga.
Mtoto wa Marehemu ,Elinewinga,Adam Elinewinga akisoma historia ya marehemu baba yake wakati wa mazishi hayo.
Mkuu wa KKKT,Dkt Fredrick Shoo akisalimiana na Waziri Ndelichako.
Mkuu wa KKKT, Dkt Fredrick Shoo akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makala.