WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteuwa Bw. Hamza Said Johari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Akitangaza uteuzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leornard Chamuriho amesema Waziri Mbarawa amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa kisheria, kifungu cha 33(1) cha sheria ya usafiri wa Anga ya mwaka 2006.
Alisema uteuzi huo umefanyika kuanzia Februari 22, 2016, ikiwa ni kuziba nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Redemptus P. Bugomola. Kabla ya uteuzi huo Bw. Johari alikuwa ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Walaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA-Consumer Consultative Council).