Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo pamoja na Mkandarasi wa Kampuni ya WABAG ya nchini India wakiwa katika mazungumzo katika eneo la mtambo wa Ruvu Juu 19 Aprili, 2017. |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiaji Prof. Kitila Mkumbo ametembelea
Mtambo wa Ruvu Juu uliopo eneo la Mlandizi Mkoani Pwani na kujionea kazi
kubwa iliyofanywa na Serikali kupitia Wizara anayoiongoza.

Akiwa mtamboni hapo alipata fursa ya kushuhudia mtambo huo ukifanya kazi kama
ilivyotarajiwa baada ya upanuzi wake kukamilika, ambapo hivi sasa mtambo una uwezo
wa kuzalisha maji safi na salama kiasi cha lita milioni 196 kwa siku.

Akizungumza baada ya kuhitimisha ziara yake Mkoani hapo, Prof. Kitila amesema kwamba ziara
hiyo ni muhimu kwake kwa kuwa amejifunza mambo mengi kuhusu namna maji
yanavyopatikana ambapo ametoa pongezi kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika
eneo hilo.

“Uwekezaji huu ni mkubwa sana uliofanyika katika eneo hili, uwekezaji huu unahitaji
kutunzawa ili kudhibti upotevu wa maji”, alisema Prof. Mkumbo.

Amewataka Mameneja wa Miradi ya Maji kuhakikisha kuwa wanajiwekea malengo katika
kuwahudumia wananchi na ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba wanayatunza
maji wayapatayo kwakuwa upatikanaji wake ni mrefu na Serikali imewekeza fedha
nyingi katika kuyapata maji hayo.

Aidha, Serikali imetekeleza mradi huo kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
Salaam (DAWASA) ambapo katika ziara yake hiyo ameweza kupita na kujionea maeneo
mbalimbali yanayozalisha maji na kuyahifadhi ikiwemo Matenki ya maji yaliyopo
eneo la Chuo Kikuu cha Ardhi yenye ujazo wa lita milioni 45, tenki la maji
safi la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10, Ruvu Darajani (In-take), Mtambo
mpya wa Ruvu Juu.

Sambamba na ziara hiyo, Prof. Kitila alipata wasaa wa kutembelea Ofisi ya Dawasco
iliyopo Kibaha na kuktana na watendaji wa ofisi hiyo akiwemo Meneja wa DAWASCO
Kibaha, Bw. Erasto Mbwambo ambaye alitoa taarifa yake kuhusu maendeleo
yaliyofikiwa katika kuhakikisha kuwa maji yanawafikia wananchi jambo ambalo
lilimfurahisha Prof. Kitila.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
(DAWASA) Bw. Romanus Mwangingo ameeleza kuwa, kwa sasa tayari maji toka Mtambo
wa Ruvu Juu yameanza kuzalishwa baada ya shughuli za upanuzi katika mtambo huo
kakamilika.

Ziara hiyo iliandaliwa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na
kuhudhuriwa na Maofisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, DAWASA,
DAWASCO, Wakandarasi pamoja na Mshauri wa mradi wa mfumo wa maji wa Ruvu Juu.