Prof Kaimenyi Ataka Kubadilishana Matokeo ya Utafiti

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya, Profesa Jacob Kaimenyi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya, Profesa Jacob Kaimenyi

Na Anne Kiruku, EANA, Arusha

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya, Profesa Jacob Kaimenyi amewataka washiriki wa mkutano wa mwaka huu wa Jukwaa la Wasomi na Sekta Binafsi kubadilishana uzoefu wa utafiti waliojifunza, hususan na watengenezaji sera.   

Prof. Kaimenyi alikuwa anazungumza katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika hoteli moja mjini Nairobi, mwishoni mwa mwiki. Ili kuweza kukuza matumizi na uoanishaji wa teknolojia katika ufumo wa uzalishaji, Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa kukuza utafiti na uvumbuzi katika taasisi za elimu ya juu.

“Vumbua au uangamie.Sisi, kama wana jumuiya ya Afrika Mashariki, hatuna budi kufanya uvumbuzi mbalimbali kama sehemu ya utendaji wetu kwa wasomi wote ili kutoa msukumo na kutoa baadhi ya mahitaji kwao kwa ajili ya kufanyiwa uvumbuzi,” alisema Prof Kaimenyi.

Katika suala ya utafiti, alisema wasomi wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali juu ya kwa nini hawafanyi utafiti kama ilivyo kwa dunia nzima. “Tunapowatuma watu wetu Marekani, Ulaya na kwingineko duniani wanaweza kushindani vilivyo na wenzao walio bora zaidi duniani.”  

Alitoa changmoto kwa wshiriki wa mkutano huo kubadilishana maarifa waliyopata na wenzao katika nchi zao. “Fanyeni yale mliyojifunza hapa kuwa sera katika nchi zenu,” alisisitiza.

Maoni ya Prof Kaimenyi yaliungwa mkono na Mwenyekti wa Baraza la Mawaziri la EAC, Prof Tarsis Bazana Kabwegyere kutoka Uganda aliyesema “unatakiwa kufanya utafiti au ujiuzulu.”

Waziri huyo aliwaambia wajumbe kwamba asilimia 84 ya vyuo vikuu nchini Ujerumani ni vya kisayansi na hivyo ndiyo sababu si ajabu kwa Ujerumani kuwa na uchumi imara barani Ulaya.
Katibu Mkuu wa EAC, Dr Richard Sezibera aliwahakikishia wajumbe waliokuwepo kwamba maazimio ya mkutano huo yatafuatiliwa kwa karibu.