Mwadui FC imebanwa mbavu kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mwadui Complex baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na maafande wajelajela Tanzania prison kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Mchezo ulikuwa wakushambuliana kwa zamu kwa timu zote na mara kadhaa washambuliaji wa timu wa timu hizo walikuwa wakishiondwa kukwamisha mipira kambani.
Matokeo ya sare ni faida kwa timu ya Prisons ambayo leo imecheza ugenini kwasababu matokeo hayo yanaifanya ifikishe jumla ya pointi 30 na kupanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya sita hadi kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa ligi nyuma ya wakata miwa wa mji kasoro bahari Mtibwa Sugar yenye pointi 33 hadi sasa.
Mwadui wao pia wanafikisha pointi 29 sawa na majirani zao Stand United lakini nao wanapanda kwa nafasi moja kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya saba hadi nafasi ya tano nyuma ya Tanzania Prisons.
Sare ya leo ni ya tatu mfululizo baada ya sare mbili kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine dhidi ya Yanga ya kufungana 2-2 badae ikafuata sare dhidi ya Mbeya City ya bila kufungana.
Mwadui hawajashinda kwenye mechi zao tatu mfululizo. Walifungwa na African Sports 1-0 jijini Tanga kisha wakafungwa tena na Azam kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Azam Complex na leo wameshindwa kutamba kwenye uwanja wao wa nyumbani.