Prime Time Promotions yatoa msaada wa chakula kwa yatima Vingunguti Dar

Pichani shoto ni Mlezi wa kituo cha kulelea Watoto waishio katika mazingira magumu kiitwacho Mwana Orphan Center kilichopo Vigunguti jijini Dar es Salaam, Mama Ummy akitoa mkono wa shukurani kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd. Juhayna Ajmi Kusaga (pichani kulia), mara baada ya kuwapelekea msaada wa vyakula mbalimbali.

Baadhi ya watoto wa kituo hicho wakisaidiana kubeba baadhi ya misaada ya vyakula iliyotolewa na Kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Uongozi wa Prime Time Promotions ukioneshwa sehemu ambayo baadhi ya watoto wa kituo hicho hulala wakati wa usiku, kama uonavyo pichani, Watoto hao hulala sehemu hiyo ya wazi kutokana na ukweli kwamba kituo hicho kimelemewa na watoto,kituo hicho mpaka sasa kina idadi ya watoto wapatao 6o, na eneo halitoshi,kutokana na hali hiyo kituo hicho bado kinahitaji msaada mkubwa wa mambo mbalimbali ikiwemo kuwapatia sehemu nyingine nzuri ya kulala watoto hao.
Pichani kati ni Mlezi wa kituo cha kulelea Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha Mwana Orphan Center kilichopo Vigunguti, jijini Dar es Salaam, Mama Ummy akielezea hali halisi ya kituo hicho kilivyoanza na kinavyojiendesha mpaka hivi sasa mbele ya Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd. Juhayna Ajmi Kusaga pichani kulia na shoto ni Meneja Mipango wa kampuni hiyo ya Prime Time, Balozi Kindamba.
Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.Juhayna Ajmi Kusaga pamoja na Mama Mlezi wa kituo hicho wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho cha Mwana Orphan Center. Kwa mtu yeyote kwa mawasiliano na kwa msaada wowote.