TIMU ya Portugal imetwaa ubingwa wa Ulaya ‘Euro 2016’ baada ya kuifunga France goli moja kwa mtungi. Portugal ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo katika dakika ya 109 baada ya mshambuliaji wake Eder kuifungia goli la shuti la mbali la kushtukiza lililomshinda mlinda mlango wa timu ya France.
Mchezaji tegemeo wa Portugal, Cristiano Ronaldo alishindwa kumalida dakika 90 za mchezo huo mkali wa fainali baada ya kujeruhiwa goti na kulazimika kwenda kutibiwa kabla ya kurudi bechi na kuanza kutoa maelekezo mithili ya msaidizi wa kocha wake, Fernando Santos.
Wachezaji wa France wataendelea kujilaumu baada ya kukosa magoli lukuki huku wakionekana kuutawala mchezo kiasi kikubwa ukilinganisha na wenzao wa Portugal.
Mchezo huo mkali ulimalizika bila kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida kabla ya kwenda kwenye dakika 30 za nyongeza hivyo Portugal kutumia vizuri dakika za dhiada.
Mchezo huo wa fainali ulikuwa na jumla ya kadi za njano 10, ambapo kadi 6 za njano zilitolewa kwa wachezaji wa Portuga huku wenzao wa France wakipata kadi 4.