Na Mwandishi Wetu, Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha linamsaka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani hapa, James Ole Millya kufuatia kauli aliyotoa kuwa Polisi imezuia maandamano ya CCM yaliyokuwa yafanyike Oktoba 9 mwaka huu jambo ambalo si kweli.
Juzi polisi mkoani hapa ilikanusha madai ya kuzuia maandamano hayo na kuongeza kwamba CCM ndiyo walioandika barua na kuiwasilisha Polisi kutaka mabadiliko juu ya ombi lao la awali.
Polisi inamsaka Mwenyekiti huyo kwa madai kuwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Arusha, uliokuwa ukiongozwa na Kaimu Mwenyekiti UVCCM ngazi ya taifa, Millya alitoa kauli kwamba Polisi iliagizwa na mtoto wa kigogo kuzuia mkutano huo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa akizungumza na waandishi wa habari jana amesema kuwa Oktoba 8 mwaka huu walipokea barua yenye kumbukumbu namba UV/Z75/1/VOL2/1/450 iliyosainiwa na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdalah Mpokwa ikiomba kibali kufanya maandamano na mkutano wa hadhara.
Kaimu huyo alisema kuwa wakati Jeshi hilo likiendelea na taratibu za
kujibu barua huyo, walipokea simu kutoka kwa katibu huyo(Mpokwa)
aliyedai kuwa wameahirisha mkutano huo. Mpwapwa alidai kuwa Jeshi hilo linamtafuta Millya kwa mahojiano ili aweze kuthibitisha kauli yake ikiwa ni pamoja na kumtaja mtoto huyo wa Kigogo aliyetoa amri kwa polisi kuzuia mkutano huo.
“Wanasiasa wanaotaka kulipaka jeshi matope hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao, na Millya tunamtafuta kupitia simu yake ya
mkononi ambayo imeita bila kupokelewa na baadaye kutokupatikana kabisa ili atueleze mtoto huyo wa kigogo aliyetoa agizo kwa polisi kuzuzia mkutano ni nani kwani sisi hatumtambui mtoto wa kigogo aliyetoa amri hiyo,” alisema Mpwapwa
Aidha katika hatua nyingine Kaimu huyo alisema kuwa CCM walifanya
mkutano pasipo kibali toka katika jeshi hilo kwa madai kuwa wakiwa
katika mchakato wa kutoa kibali walipigiwa simu na Katibu wa UVCCM
kuwa wameahirisha mkutano huo.
Kauli hiyo ya Kaimu Mpwapwa inatofautina na hali ilivyokuwa wakati wa
Mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika eneo la Hospitali ya
Mtakatifu Thomas, kwa sababu siku ya mkutano huo Jeshi la polisi
likiongozwa na Mkuu wa Polisi wialya ya Arusha Zuberi Mwombeji pamoja na askari walikuwa katika mkutano huo wakiangalai hali ya usalama.
Akizungumzia suala hilo Mpwapwa alidai kuwa Mkuu huyo wa kituo pamoja na askari walilazimika kufika eneo la mkutano ila walipokuta mkutano umeshaanza walishindwa kuuzuia wakihofia hali ya usalama kwa wananchi waliokuwa katika eneo la tukio hilo. Kaimu huyo alitoa onyo kwa vyama vya siasa, kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na si kujichukulia sheria mkononi.
Inadaiwa kuwa chanzo cha mvutano huo uliosababsiha kuzuiwa kwa
maaandamano hayo ambayo baaadaye yaliruhusiwa kufanyika ni mgogoro unaodaiwa kuwa ndani ya UVCCM katika Wilaya ya Arusha, ambapo baadhi ya viongozi wa umoja huo wanadaiwa kupinga ziara ya viongozi hao wa kitaifa huku wengine wakipinga ziara hiyo ifanyike.
Aidha Kaimu huyo alipoulizwa kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Jeshi
hilo dhidi ya CCM ambao walifanya mkutano pasipo kibali, alisema kuwa
wanawapa onyo huku katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, viongozi wa ngazi za juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakishtakiwa kwa kosa la kufanya mkutano wa hadhara na maandamano pasipo