DIWANI wa Kata ya Tunduma, Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na Mchungaji wa Kanisa la KKKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu katika eneo hilo.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 3; jana asubuhi katika eneo hilo la Tunduma mara baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .
Amesema mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Amesema suala hilo limegubikwa na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini.
Amesema kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.
Amesema shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.
Hata hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.
Kufuati hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.
Picha na Mbeya yetu