Polisi Wawapiga Mabomu ya Machozi Wabunge Bungeni

Jengo la Bunge la Wawakilishi Nigeria

Jengo la Bunge la Wawakilishi Nigeria

POLISI wa Mji Mkuu wa Lagos, nchini Nigeria, wamefyatua gesi ya kutoa machozi ndani ya Jengo la Bunge, na kulazimisha kuahirishwa kwa mjadala muhimu wa bunge hilo kuhusu kurefushwa kwa kipindi cha hali ya tahadhari Kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa za mwaandishi wa habari hizi inaeleza kuwa maofisa wa Polisi walikuwa wakijaribu kumzuia Spika wa Bunge la Wawakilishi, Aminu Tambuwal ambaye alihamia Chama cha Upinzani mwezi uliopita kuendelea na mjadala huo.

Wabunge wa upinzani wanasema kuwa hali ya tahadhari imeshindwa kuhimili visa vya wapiganaji wa Kiislam wa Boko Haram. Hata hivyo anaongeza kuwa Ofisa Mkuu wa Polisi ametakiwa kufika mbele ya Baraza la Senate kuelezea hatua hiyo ya maofisa wa polisi kurusha mabomu ya machozi ndani ya Bunge. Bunge limefungwa hadi juma lijalo.

-BBC