JESHI la Polisi limetangaza kutoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi juu ya wavamizi wa Kituo cha Polisi Stakishari kilichopo eneo la Ukonga ambao waliuwa raia na askari wanne kabla ya kupora baadhi ya silaha kituoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Jeshi la Polisi litamzawadia kiasi hicho cha fedha mtu atakayetoa taarifa sahihi na kufanikiwa kupatikana kwa wavamizi wa kituo hicho.
Alisema kiasi hicho cha fedha watakitoa ikiwa ni dhana ya kuongeza ushirikiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na raia wake. Juzi majira ya saa nne usiku watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia kituo cha Polisi Stakishari cha jijini Dar es Salaam na kuua askari na raia waliokuwa kituoni hapo kabla ya kuvunja ghala la kuhifadhia silaha kituoni hapo na kutokomea na silaha kadhaa. Askari waliopoteza maisha ni pamoja na Koplo Gaudin, Sajenti Adam (Mara), Kapteni Peter (Geita) na Konstebo Anthony