Polisi Kilimanjaro wakamata wahamiaji haramu 42

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema

Na Mwandishi Wetu, Moshi

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wahamiaji haramu 42 kutoka nchini Ethiopia na Somalia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz alisema wahamiaji hao walikamatwa Julay mbili majira ya saa kumi jioni katika eneo la Kilototoni Himo wilayani Moshi.

Kulingana na taarifa ya kamanda Boaz Raia hao wa Ethopia na Somalia waliingia nchini kinyemela kupitia njia za panya na kwamba walikuwa wamejificha kwenye nyumba ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kwa jina.

Alisema Raia hao waliingia nchini bila kuwa na vibali vya kuwaruhusu kuingia nchini na kwamba walikamatwa baada ya wananchi wema kutoa taarifa polisi kuhusiana na raia hao kuwepo maeneo hayo.

Alisema katika kundi hilo la wahamiaji haramu 39 ni Raia kutoka nchini Ethiopia na wengine watatu ni kutoka nchini Somalia. Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Abahamu Lamango, Dauji Elius, Terepes Lombebo, Eliso Ashe, Wolde Abuye, Muluneh Warko, Endele Mekengo, germelo Adero, Adamsu Yoikobo wote (25)

Wengine ni Ahamdin Mohamed, Tamraji anor, Fanus Krew, Dive Man, Taganye Phawuls, Tamama mekeyo, Masale Cufomo wote wakiwa na umri wa miaka 24 na Taregna Mengehah, Dembalo Adrea, Tarefa Abulee, Biranus Yohanis, Melese Gemeda, Denekel Kebeda, Mulunhe Danabo, Abyenh Landebi wote wenye umri wa miaka 22.

Abaine Lomore, Mesifin Mundido, Rebeba kofiso, Maratu Kabiro, Kasahun Acio, Fayhisa Lete, Budeta Beketa wote wakiwa na umri wa miaka 23 na kuongeza kuwa Bayonse Gernagano, Abeda Livanso, Seleman Himranm, wote wakiwa na umrei wa miaka 26.

Kamanda Boaz aliwataja wewngine kuwa ni Mamushi De Sita (28), na Keboda Mudamo, Yohanis Watharo ro(30) Kadri Amiri (18) wote raia wa Ethiopia na Raia wa Somalia ni pmoja na Mohamed Hasani (24) Mohamed Alii (28) na Rawud hasani (26).

Hata hivyo Kamanda Boaz hakuweza kuweka wazi kuwa raia hao waliingia nchini lini licha ya kueleza kuwa wameingia kwa kupitia njia zisizo sahihi na kwamba taratibu za kisheria zinafanyika ili kuweza kuwafikisha mahakamani.