Polisi Dar Wakamata Matapeli, Walimteka Raia na ‘Furushi’ la Fedha

Gari la Polisi likiwa limezuia (piga pini) barabara ya Mtaa wa Azikiwe Posta Mpya kuzuia moja ya gari linalosadikika kutumiwa na matapeli kumteka raia mmoja na fedha zake.

 

Matapeli wakishushwa kwenye gari walilokuwa wakilitumia na kupandishwa kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa

Matapeli wakishushwa kwenye gari walilokuwa wakilitumia na kupandishwa kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa

POLISI Dar es Salaam leo wamefanikiwa kuwakamata watu wanaosadikiwa kuwa matapeli eneo la Posta Mpya Mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam ambao walimteka raia mmoja akiwa na fedha kisha kumuingiza kwenye gari ndogo na kutaka kutokomea naye kusiko julikana. Hata hivyo mtego huo ulistukiwa na baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa walianza kuwafuatilia kwa kuwasiliana na wanausalama waliopo maeneo mbalimbali ya jiji na kufanikiwa wakamata baada ya kuzuiwa (ku-pigwa pini kwenye foleni ya magari) na gari la polisi.

 

Polisi wakiondoka eneo latukio huku wakiwa wamewakamata wahusika na kulichukua gari lililotumika (nyuma)

Hili ndilo gari lililotumiwa na matapele kumteka muhusika

Polisi waliokuwa wakilifuatilia gari hilo nao wakiondoka eneo la tukio huku wakiwa ‘standby’ kwa lolote, bunduki mkononi.