Polis Arusha Waweka Mbinu Mbeya Kudhibiti Uharifu

kamanda

Na; Magesa Magesa,Arusha

POLISI mkoani hapa imesema bila ushirikiano madhubuti kutoka kwa wananchi katika kuimarisha ulinzi Jeshi la Polisi pekee haliwezi kutimiza hazma hiyo hivyo kuwataka wananchi kuwa waangalifu kwa kutoa taarifa zinazoashiria uvunjifu wa amani kwenye mitaa yao ili lishughulikiwe.

Aidha uanzishwaji wa mafunzo ya polisi jamii katika mitaa ni dhana itakayosaidia kwa kiasi kikubwa udhibiti wa matukio ya kiuhalifu yanayofanywa na baadhi ya watu wachache wenye nia mbaya.

Katika hafla ya uzinduzi wa vituo vya polisi jamii katika mitaa minne iliyopo katika kata ya moivaro jijijni arusha kamanda wa polisi wilaya ya arusha Emanueli Marcko Tille alisema jeshi la polisi limeamua kuanzisha mafunzo ya polisi jamiii kwa lengo la kusaidia kupunguza matukio madogo yanayotokea ndani ya jamii hivyo kama msimamizi mkuu atahakikisha polisi hao wanafamya kazi katika jamii bila kuwepo lawama.

Tille alisema kuwa licha ya kuwepo kwa maeneo korofi yaliyokothiri kwa matukio ya wizi na ujambazi polisi hao watakuwepo katika mitaa yao wakifanya ulinzi nyakati za usiku huku wakishirikiana na mjeshi la polisi kuhakikisha ulinzi na usalama unadumishwa sehemu ya makazi ya watuu kwani asilimia kubwa ya uhalifuu unafanywa katika mitaa.

“Matukio mengi yanayotokea yamekuwa ni miongonimwa jamii hivyo ni vyema sisis kama jeshi la polisi tuanahakikisha tunawaweka wasaidizi katika kila mitaa kufanya doria ili kuhakikish raia na mali zake wapo salama”

Diwani wa kata hiyo ya Moivaro ,Erick Moiro alisema katika kata hiyo wanachangamoto yagari la doria nyakati za usiku hvyo kupelekea kukwamisha kazi pindi wanapowakamata wahaalifu nyakati za usiku hivyo alilipomba jkeshi la polisi kufanya jitihada za dhati ili kufanikisha hilo.