Michel Platini atajiuzulu kuwa rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya – UEFA baada ya mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo kukubali aendelee na adhabu yake
Michel Platini atajiuzulu kuwa rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA baada ya mahakama ya upatanishi katika michezo CAS kuamua kukubali aendelee na adhabu yake ya kupigwa marufuku kujihusisha na shughuli za uongozi wa michezo, lakini adhabu hiyo imepunguzwa kutoka miaka sita hadi miaka minne.
Platini mwenye umri wa miaka 60 mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa , atawasilisha barua yake ya kujiuzulu katika mkutano mkuu wa shirikisho hilo, wamesema mawakili wake katika taarifa.
Platini amesema uamuzi huo ulikuwa ukiukaji mkubwa wa haki, na ataendelea kutafuta haki yake katika mahakama za Uswisi.