WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda tayari amekabidhi sh. milioni 10 kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwa ni ahadi yake aliyotoa kwa Taifa Stars ikiwa ni motisha kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mechi yao na Chad iliyochezwa Novemba Mosi mwaka jana jijini N’Djamena.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso linaanda orodha ya wachezaji wanaostahili kunufaika na ahadi hiyo, na baadaye kuiwasilisha BMT kwa ajili ya mgawo kwa wahusika.
Tunamshukuru Waziri Mkuu Pinda kwa ahadi hiyo, kwani Taifa Stars ilifanikiwa kushinda mechi hiyo ya ugenini mabao 2-1, ushindi ambao bila shaka ulichagizwa na ahadi hiyo.
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Desemba 30 mwaka jana ilijadili masuala mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo malalamiko juu ya kuuzwa kwa timu ya Small Kids ya Rukwa.
Usikilizaji wa suala hilo uliahirishwa na Kamati kuagiza kwanza ipatiwe vitu vifuatavyo; Katiba iliyosajiliwa ya Small Kids, muhtasari (minutes) na uamuzi wa kikao chochote kilichofanyika
Wakati huo huo Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji itatuma wajumbe wake wawili Tabora kukutana na Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA).
Wajumbe hao katika kikao chao na Kamati ya Utendaji ya TAREFA watasikiliza kuhusu kiini cha mgogoro uliopo na baadaye watawasilisha taarifa kwa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji. Kamati itafanyia kazi ripoti hiyo kabla ya kufanya uamuzi.