KWA kile kumjali mteja na Mtanzania kwa ujumla kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni za kutoa elimu kwa raia wanaotumia vinywaji (bia aina mbalimbali zinazozalishwa na SBL), ili wanywe kistarabu bila athari yoyote.
SBL inaamini wapo baadhi ya wateja wake na raia wengine ambao wamekuwa wakijisahau katika matumizi ya pombe jambo ambalo limekuwa likiwagharimu wao, familia zao na hata taifa kwa ujumla.
Unywaji wa pombe ni mzuri kwa wenye sifa na wanaotumia kinywaji hicho, lakini endapo mtumiaji atakunywa kistarabu. Ndio maana SBL imeamua kutoa elimu kwa umma juu ya Unywaji wa Pombe Kistarabu.
Zifuatazo ni picha anuai katika Uzinduzi wa Kampeni za Kunywa Kistarabu;-