Mtaalamu kutoka kitengo cha Mazingira katika Wizara ya Nishati na Madini Bw Silinge akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nishati na Madini Prof. Abdulkarim Mruma (kushoto) ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania.
Bi Carlotta Richter kutoka Tanzania Renewable Energy Association (TAREA) akimwonyesha moduli ya umeme nuru Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nishati na Madini Prof. Abdul karim Mruma ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (kushoto).
Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nishati na Madini Prof. Abdul karim Mruma ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (kushoto) akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhusu umeme wa jua.
Baadhi ya wananchi wakiangalia gari linalotumia gesi asili kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwenye maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nishati na Madini Prof. Abdul karim Mruma (kushoto) ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania akiwaeleza wanahabari jinsi alivyofurahishwa na Maonesho ya Wiki ya Nishati na Madini hasa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) walivyoshirikisha watu binafsi kuonyesha shughuli zao. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Nishati na Majini)