Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Danny Mwakiteleko, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa msafara wa mazishi kuelekea Mbeya.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakiwa wamejipanga kabla ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Mwakiteleko nyumbani kwake Tabata Chang’ombe.
Baadhi ya wambolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu, Mwakiteleko.
Waziri Emmanuel Nchimbi akiwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu kwenye msiba huo jana jioni.
Msafara wa waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa marehemu kuelekea kwenye magari ambayo yalisafirisha mwili kuelekea Mbeya kwa mazishi.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Ltd, Deodatus Balile (aliyevaa suti nyeusi katikati) akijadiliana jambo na baadhi ya waombolezaji muda mfupi kabla ya safari ya kuelekea Mbeya kwa mazishi ya Mwakiteleko, kushoto ni Mhariri wa Habari wa Mtanzania, Jacton Manyerere. (Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog)