
Washiriki wa mkutano wa tamasha la jinsia tanzania 2013 wakiandamana kuingia katika viwanja vya TGNP kabla ya kuanza kwa maadhimisho. Maadhimisho hayo yanaenda sambamba na kusherehekea miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi za mtandao huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Ussu Mallya akizungumza kuwakaribisha wageni mbalimbali katika tamasha hilo na kutoa machache juu ya miaka 20 ya harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi za TGNP.


Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Bi. Mary Rusimbi akizungumza kwenye mkutano wa Tamasha la Jinsia Tanzania 2013.



Baadhi ya wageni kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifa wakifuatilia matukio anuai katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2013.





Watu wenye ulemavu wa kusikia wakielezewa kwa kutumia ishara masuala anuai yanayiowasilisha katika tamasha.







Wakati mwingine burudani zilipozidi washiriki walishindwa kuvumilia na kujikuta wakiingia kati na kusakata rumba. Vikundi mbalimbali vya muziki na sanaa vilikuwa vikiburudisha.


Washiriki kutoka mikoa anuai wakijisajili kabla ya kuanza ushiriki wa Maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Tanzania Jijini Dar es Salaam


Kundi la wasanii wa Parapanda wakifanya igizo kuonesha jamii ya wanawake inavyonyanyasika katika maeneo ya ajira.
