Philip Mangula Arudi Kileleni CCM, Achaguliwa Makamu Mwenyekiti Bara

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akizungumza na Makamu Mwenyekiti Bara CCM, Phili Mangula (kulia) na Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) Picha na Ikulu.

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa CCM zamani, Philip Mangula hatimaye amerudi katika nafasi ya juu ya uongozi wa CCM baada ya kuchaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara kwa kura 2397. Hata hivyo wakati kiongozi huyo akifanikiwa kuchakuwa nafasi hiyo, Rais Jakaya Kikwete ametetea nafasi yake tena kwa kishindo baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama hicho kama Mwenyekiti wa Taifa kwa kura 2395 kati ya kura 2397 zilizopigwa.

Wengine waliofanikiwa kutetea nafasi zao ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein aliyechaguliwa tena kuwa Makamu Mwenyekiti CCM upande wa Zanzibar baada ya kujizolea kura zote 2397.

Wajumbe 10 wa NEC waliopita pamoja na kura zao kwenye mabano ni; Stephen Wassira (2,135), January Makamba (2,093), Mwigulu Nchemba (1,967), Martine Shigela (1,824), William Lukuvi (1,805), Bernard Membe (1,455), Mathayo David Mathayo (1,414), Jackson Msome (1,207), Wilson Mukama (1,174), pamoja na Fenela Mukangara (984).