Perfect Lady Salon Yawapamba Washiriki Epiq Bongo Star Search 2012

Wafanyakazi wa Perfect Classic Salon wakiwasuka na kuwapamba washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 katika jumba lao lililopo jijini Dar.

 Mkurugenzi wa Perfect Classic Salon (kati mwenye nguo nyeusi) Bi. Ester Kiama akitoa maelekezo kwa mmoja ya wafanyakazi wa Salon yake jinsi ya kumtengeneza mshiriki wa Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012). Perfect Classic Salon imedhamini shindano hilo kwa kuwapendezesha washiriki na kuwapa muonekano mpya wanapokuwa wakiimba stejini.
 Mwanadada Kulwa ambaye ni mtaalamu wa kusuka kutoka Perfect Classic Salon akiwajibika.
Nae mwanadada Sabrina ambaye ni mtaalamu wa kushona nywele za akina mama (Weaving) akiwajibika.

Na Mwandishi Wetu

PERFECT
Lady Salon imeingia katika udhamini wa Shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBBS) kwa kuwapamba na kuwapa muonekano mpya washiriki wote wanaoshiriki kwenye kinyanga’anyiro hicho cha kumtafuta taa mwenye kipaji cha kuimba nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kuwatambulisha wadhamini uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Perfect Lady Salon, Bi. Ester Kiama alisema kuwa ikiwa yeye ni Mtanzania anayependa maendeleo ya vijana ameona ni vyema kujitoa kudhamini shindano hilo kwa kuwapa washiriki muonekano mpya.

“Nafurahi sana kuungana na Bi. Ritta Poulsen kudhamini shindano hili linalovumbua vipaji vya vijana ambapo mimi, nimechukua upande wa kuwapamba washiriki na kuwapa muonekano mpya wawapo stejini,” alisema Ester Kiama.

Hata hivyo aliongeza kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuungana mkono pale unapoona mtu anafanya jambo linaloleta maendeleo katika nchi yetu. Pia Bi. Ester Kiama alisema, Perfect Lady Salon imefungua milango kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya kazi na nao, asisite kuwasiliana nao wanapatikana Kinondoni mkabala na Chuo Kikuu Huria.

Shindano la EBBS linaloshirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani linaendelea ndani ya Kituo cha Televisheni cha ITV na sasa washiriki wamefikia katika hatua ya mtoano