RAIS wa Rwanda Paul Kagame amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliopita na tume ya uchaguzi nchini humo kulingana na habari zilizotolewa. Taarifa zinasema kwamba tume hiyo ilimuongezea rais Kagame asilimia ya kura alizopata kutoka 98.63, ikiwa ni takwimu zilizotangazwa hapo awali hadi asilimia 98.79. Katika uchaguzi huo Kagame alichuana na wapinzani wawili, ambapo hakuna hata mmoja wao aliyefanikiwa kupata asilimia moja ya kura.
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda ilisema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo. Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.