Na; Binzubeiry.co.tz
TIMU za Mbeya City na Mwadui FC zimetinga Robo Fainali ya Kombe ka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya ushindi wa nyumbani leo.
Prisons imewafunga ndugu zao, Mbeya City mabao 2-1 Uwanja wa Sokoine, huo ukiwa mchezo wa pili mfululizo timu hiyo inapoteza chini ya kocha Mmalawi, Kinnah Phiri baada ya Jumatano kufungwa 3-0 na Azam katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Prisons walianza kupata bao dakika ya 39 kupitia kwa mshambuliaji wake, Mohammed Mkopi aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Sam Kimenya, kabla ya Mbeya City kusawazisha kupitia kwa Joseph Mahundi dakika ya
Shujaa wa Priosns alikuwa ni kipa wake, Benno Kakolanya aliyefunga bao la ushindi dakika ya 82 baada ya kupiga mpira mrefu kutoka langoni mwake baada ya mchezaji wa City kuotea na mpira huo kumpita kipa Mganda wa Mbeya City, Hannington Kasyebula ambaye alikuwa amesogea mbele ya lango lake.
Uwanja wa Mwadui Complex, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerson John Tegete amefunga mabao mawili, Mwadui FC ikiilaza 3-1 Rhino Rangers ya Tabora. Bao lingine la Mwadui limefungwa na Rashid Mandawa.
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili ya hatua ya 16 Bora, Simba SC wakiikaribisha Singida United Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, wakati Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wenyeji Toto African wataikaribisha Geita Gold ya Geita.
Mechi za 16 Bora ya michuano hiyo, zitahitimishwa keshokutwa kwa mchezo mmoja, kati ya wenyeji Panone FC dhidi ya Azam FC ya Dar es Salaam Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Prisons na Mwadui zinafanya idadi ya timu zilizotinga Robo Fainali za michuano hiyo hadi sasa kufika nne, baada ya Yanga kuitoa JKT Mlale kwa kuifunga 2-1 Februari 24, Ndanda FC kuwatoa waliokuwa wanashikilia taji, JKT Ruvu kwa kuwafunga 3-0 na Coastal Union iliyoifunga 1-0 Mtibwa Sugar juzi.
MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA TFF
Februari 24, 2016
Yanga SC 2-1 JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
Februari 26, 2016
Ndanda FC 3-0 JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara)
Coastal Union 1-0 Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
Februari 27, 2016
Mwadui FC 3-1 Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga)
Prisons 2-1 Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
Kesho; Februari 28, 2016
Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam)
Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
J’tatu Februari 29, 2016
Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)