KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Farncis amewasili nchini Sri Lanka kwa ziara ambako anatarajiwa kusisitiza umhimu wa mazungumzo baina ya makundi mbalimbali ya imani hasimu za kidini nchini humo.
Pamoja na hayo, Papa Francis akiwa nchini humo anatarajiwa kuhimiza suala la maridhiano wakazi walio wengi wa visiwa vya Sinhalese na wale wachache wa kisiwa cha Tamil. Hii ni ziara ya kwanza kwa Papa Francis kutembelea taifa hilo tangu ziara ya kwanza ya Papa ya mwaka 2009 ifanyike. Rais wa sasa wa Sri Lanka Maithripala Sirisena ameahidi kukomesha ubaguzi wa kidini visiwani humo.
Wakati huo huo; Serikali ya Angola inasema kuwa uamuzi umechukuliwa na mataifa ya Afrika kuingilia kijeshi harakati za waasi wa kihutu kutenda uhalifu Mashariki mwa Congo. Afisaa mmoja mkuu (Joaquim do Espirito Santo) anasema kuwa mkutano wa kikanda uliotarajiwa kufanyika leo, umefutiliwa mbali kwa sababu ya hofu ya kuchelewesha mipango ya kijeshi dhidi ya waasi hao.
Umoja wa mataifa ulithibitisha mwishoni mwa wiki jana kwamba waasi wa FDLR wamepitwa na muda waliowekewa wa mwisho kwao kusalimisha silaha. Wiki jana Rais wa DRC, Joseph Kabila, aliambia katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupambana na waasi hao. Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa, (Martin Kobler) amesema kuwa hatua za kijeshi ndizo pekee zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya waasi hao kwa sasa.
-BBC