Panone Fc, Alliance Uso Kwa Uso FDL

PANO

TIMU za Abajalo, Ashanti United za Dar es Salaam zimepangwa pamoja na African Sports ya Tanga katika Kundi Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara.

Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes msimu wa 2016/2017. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu mara baada ya kukamilisha mchakato wa usajili unaoanza Juni 15, 2016.

Kila Kundi lina timu nane na timu nyingine katika katika Kundi A ni Kiluvya United ya Pwani, Friends Rangers ya Dar es Salaam, Lipuli ya Iringa, Mshikamano FC ya Dar es Salaam na Polisi Dar ya Dar es Salaam
kundi B lina timu za JKT Mlale ya Ruvuma, Coastal Union ya Tanga, Kimondo FC ya Mbeya, Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam, Kurugenzi ya Iringa, Mbeya Warriors ya Mbeya,. Njombe Mji ya Njombe na Polisi Morogoro ya Morogoro.

Kundi C lina timu za Alliance Schools ya Mwanza, Mgambo Shooting ya Tanga, Mvuvumwa FC ya Kigoma, Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya Dodoma, Polisi Mara ya Mara, Rhino Rangers ya Tabora na Singida United ya Singida