PAMOJA NA TUHUMA ZA KUCHAKACHUA,MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI!

Tangazo rasmi limetolewa kuthibitisha kuwa Rais Museveni wa Uganda ndiye mshindi katika uchaguzi uliofanyika Ijumaa nchini humo. Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Yoweri Museveni alishinda kwa asilimia 68, katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Ijumaa. Naye mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alipa asilimia 26ya kura. Bw. Besigye alikataa matokeo hayo na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika zoezi zima la uchaguzi. Chama kilicho madarakani kimetuhumiwa kwa kutumia rasilimali za serikali kuwahonga wapiga kura.

Picha na habari kwa hisani ya Michuzi blog.