KATIKA kuhakikisha inaendelea kutimiza ahadi zake za kuwazawadia wateja wake, kampuni ya Samsung Tanzania imefanya hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya nne katika promosheni inayoendelea ijulikanayo kama Pambika na Samsung yenye lengo la kupambana na bidhaa feki kwa kuwazawadia wateja wanaonunua bidhaa halisi.
Mshindi wa kwanza wa droo ya nne ya Pambika na Samsung, Bw. Hasmin Karim, alielezea furaha yake mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Mashine mpya ya kufulia nguo katika tukio hilo lililofanyika katika maegesho ya magari ya Quality Center jijini Dar es salaam.
Bw. Hashim alisema kwamba “Nawashukuru na kuwapongeza Samsung Tanzania kwa promosheni hii ya kuwazawadia wateja wake wanaonunua bidhaa halisi na kuzisajili Kwani inatoa hamasa kwa watu kutonunua bidhaa feki lakini pia naisifu kampuni Samsung kwa kutengeneza bidhaa zinazokidhi haja ya kila mmoja”.
Pambika na Samung imeanza rasmi Septemba 7, 2013 na inaendelea mpaka Desemba 23, 2013 ikiwa na lengo la kutoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Milioni 100, zawadi hizo ni Luninga za LED 32’, Kompyuta mpakato, Jokofu, Muziki wa nyumbani, Samsung Tablet, Mashine za kufulia nguo, pamoja na deki za DVD huku zawadi kubwa ya mwisho ikiwa ni gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin itakayosheheni bidhaa za Samsung.
Mpaka sasa, washindi 60 tayari wameshajinyakulia bidhaa mbalimbali toka kuanza kwa promosheni hii ambapo droo tatu za kila wiki tayari zimeshafanyika. Wateja 21 wameshajishindia deki za DVD kila mmoja na wateja 13 wameshajishindia Muziki wa nyumbani. Majiko 12 ya kupashia chakula na majokofu matatu yameshapata washindi huku wateja wawili wameshajinyakulia Galaxy Tab 10.1. Zawadi nyingine ni Kopmyuta mpakato nne, Luninga za LED 32’ nne na mashine ya kuoshea nguo moja tayari zimeshatoka ndani ya wiki nne za promosheni hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara aliwapongeza washindi wote na kuwahamasisha watanzania kuchangamkia nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali katika promosheni ya Pambika na Samsung kwa kununua bidhaa halisi za Samsung na kuongeza bidhaa muhimu katika nyumba zao huku wakifaidika na huduma za dhamana kwa miezi 24 kwa bidhaa za Samsung.
Hata hivyo, Bw. Manyara aliwashauri wateja kuwa makini ili wasiweze kuhadaika na watu wanaouza bidhaa feki ambao wanatumia udhaifu wa wateja kutojua sheria za biashara zinazolinda haki za mteja na kutumia njia zisizo halali kuwadhulumu Watanzania wasiokuwa na hatia.
Mshindi wa pili wa droo ya nne ni Athumani Amiry Lyana (32) mkazi wa Dar es salaam ambae ni Mkaguzi ofisi ya Ukaguzi ya Taifa aliyejinyakulia Luninga ya LED ya inchi 32 huku Mshindi wa tatu ni Amina Mlula (28) mkazi wa Dodoma ambae ni muuza duka aliyejishindia Kompyuta mpakato.
Washindi wengine wa wiki hii ni Martha Richard Mushi (27) Moshi, Sadiki Hussein Katau (58) wa Dar es salama, Rosalia Madereke (66) kutoka Dar es salaam waliojishindia jiko la kupashia chakula kila mmoja. Washindi wa Muziki wa nyumbani kila mmoja ni Praygod Amos Nnko (39) Arusha, Richard Kayombo Marcelino (44) Dar es salaam, Francis Mnyema Bernatus (28) na Dar es salaam.
Wengine ni Charles Faustine Chacha (29) Dar es salaam, Issa Mohamed Shami (45) Dar es salaa, Mohemmed Abdallah Kheriz (44) Dar es salaam, Devota Richard Nyato (20) Mbeya, na Mkazi wa Mwanza James Mizanza Kedela (53) wote wamejishindia deki za DVD toka Samsung.
Kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kushinda, unatakiwa kununua bidhaa yoyote halisi ya Samsung. Kama umenunua simu ya mkononi utatakiwa utume tarakimu 15 za utambulisho wa simu yako yaani namba za “IMEI” kwenda 15687. Na kama umenunua bidhaa nyingine yoyote ya Samsung basi utatakiwa ujaze fomu Maalum zinazopatikana katika maduka yote ya Samsung nchi nzima.