Pambika na Samsung Yajiandaa Kumzawadia Mteja Gari Jipya

Akizungumza na wanahabari Meneja wa Samsung Tanzania kitengo cha mauzo na Usambazaji Bw Sylvester Manyara akizungumza na wanahabari akiwahimiza Watanzania kuzidi kununua bidhaa halisi na kuzisajili katika mfumo wa dhamana ya ziada na kuingia kwenye droo ambapo bado nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya Mitsubishi Double Cabin ipo wazi katika droo itakayofanyika Jumatatu ya wiki ijayo katika maegesho ya magari ya Mlimani City, Dar es salaam.

Meneja wa Samsung Tanzania kitengo cha mauzo na Usambazaji Bw Sylvester Manyara akizungumza na wanahabari walipokuwa wakitafuta washindi wa  droo ya wiki ya tano ya Pambika na Samsung. Kushoto ni Mratibu wa Promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na msimamizi toka bodi ya kusimamia michezo ya bahati nasibu Tanzania Bw. Bakari Maggid.

Mratibu wa Promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew (kushoto) akichezesha droo ya wiki ya tano ya Pambika na Samsung kutafuta washindi 15, kulia ni msimamizi toka bodi ya kusimamia michezo ya bahati nasibu Tanzania Bw. Bakari Maggid kifuatilia kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na washindi wanapatikana kwa njia sahihi. Kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania.

PROMOSHENI ya wiki sita ya pambika na Samsung inayoendelea imetangaza majina ya washindi wa droo ya tano katika droo ya wiki hii iliyofanyika makao makuu ya Samsung na kushuhudia wateja 15 wakijishindia zawadi mbalimbali na kufanya jumla ya wateja 75 kuzawadiwa ndani ya wiki tano tangu kuanza rasmi kwa promosheni hii Septemba 7, 2013.

Samsung itafunga pazia la mwisho la promosheni ya Pambika na Samsung wiki ijayo Jumatatu ya Desemba 23, 2013 ambapo mteja mmoja mwenye bahati ataweza kujiondokea nyumbani na zawadi kubwa ya gari aina ya Mitsubishi Double Cabin itakayosheheni bidhaa zote zilizokuwa zikitoka kila wiki toka Samsung.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo ya tano ya kila wiki ya Pambika na Samsung, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara aliwahimiza watanzania kuwa makini na bidhaa feki kwani zinaharibu thamani ya maisha yao na badala yake waendelee na utamaduni wa kununua bidhaa halisi na kuzisajili hata mara baada ya kumalizika kwa promosheni ya Pambika na Samsung.

Manyara alisema kuwa “Sisi Samsung tumefurahishwa na mwenendo mzima wa droo za kila wiki zinazofanyika chini ya uangalizi na sheria za Bodi ya michezo ya kubahatisha, tukiwa tunaelekea katika droo yetu ya mwisho ya kutoa zawadi kubwa kabisa ya gari ambayo ni Mitsubishi Double cabin iliyoseheni bidhaa za Samsung, naomba nimuhamasishe kila mtu kuendelea kununua na kusajili bidhaa halisi za Samsung kutoka kwenye maduka yetu au mawakala waliothibitishwa na Samsung wanaopatikana nchi nzima”.

“Lengo letu kuu si kuongeza mauzo ya bidhaa zetu ila ni kutengeneza jukwaa litakalohamasisha watanzania wote kufahamu tatizo la bidhaa feki zilizo sokoni, Samsung ina jukumu hili la kijamii la kuwalinda wateja wake kutokana na bidhaa feki, tumeleta Pambika na Samsung ili kubadili maisha ya wateja na kuwafanya wawe na furaha pamoja na familia zao pale wanaponunu bidhaa halisi na kuzisajili katika mifumo yetu ya dhamana ambao haipatikani kwenye bidhaa feki” alielezea Bw Manyara.
Baadhi ya washindi wa wiki hii waliojishindia zawadi mbalimbali ni Adam Kennedy Manene (17) Mwanza ambae ni Mwanafunzi wa Shule ya sekondari aliyejishindia deki ya DVD, Kija Shija (22) kutoka Dodoma aliyejishindia Muziki wa nyumbani, mwengine ni kutoka Mbeya aliyejishindia deki ya DVD Docus Moses (22) mfanyabiashara wa jijini Mbeya na Shamasa Said Hamis toka Arusha aliyejishindia zawadi Muziki wa Nyumbani.

“Bidhaa za Samsung zina ubora wa kimataifa na zinahakikisha ubora huo kwa kudumu muda mrefu lakini kuna bidhaa feki sokoni ambapo changamoto yake ni ugumu wa kutofautisha na bidhaa halisi, mamlaka husika pamoja na wadau wakubwa tunatakiwa kufanya kazi ya ziada katika kumkomboa mtumiaji wa mwisho aweze kufurahia thamani ya bidhaa anayonunua” alimalizia Bw Manyara
Toka kuanza kwa Pambika na Samsung tayari imeshazawadia wateja mbalimbali 75 ambapo zawadi zilizotoka ni Kompyuta mpakato 5, Majiko ya kupashia chakula 15, Luninga za LED 32’, muziki wa nyumbani 16, Samsung Galaxy Tab 3, mashine za kufulia nguo 2, jokofu 3, na deki za DVD 27 ndani ya wiki tano kwa washindi toka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro na Kilimanjaro.

Kuingia kwenye droo na kujihakikishia nafasi ya kushinda, mteja atatakiwa kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajiili katika mfumo wa dhamana ya ziada kwa kutuma nambari za utambulisho wa simu hiyo yaani namba za “IMEI” kwenda 15685, na kwa wale watakaonunua bidhaa nyengine watatakiwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika maduka yote ya Samsung ambapo wataingia kwenye droo na kuwa na nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya Mitsubishi Double Cabin katika droo ya mwisho itakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu ya Desemba 23, 2013.