BONDIA Rashid Matumla na Patrik Omot wa Kenya wanategemea kupanda ulingoni kesho katika Ukumbi wa Makonde mkoani Mtwara. Mabondia wote wamepima uzito na taarifa ni kwamba wote wana uzani sawa wa kilo 73, na afya njema huku kila mmoja akimtambia mwenzake.
Shughuli ya upimaji iliyoendeshwa na Katibu Mkuu wa TPBO, Ibrahim Kamwe pamoja na daktari Madono lilienda vema. Taarifa zaidi zinasema kabla ya mpambano huo kutakuwa na mapambano ya utangulii, ambapo bondia Bakari Mohamed wa Mtwara na atazichapa na Abdalah Mohamed wa jijini Dar es Salaam katika pambano la ubingwa kg 57, pambano lingine itakuwa kati ya mabondia toka kambi ya Black Mamba ya Mtwara na mabondia toka kambi ya Dar es Salaam.
Bondia Haruna Mnyalukolo atacheza na Ashraf Abdala, Issa Matumla (mtoto wa Rashid Matumla) atacheza na Hamis Mtupeni, Hamis Ali Mkupa wa Mtwara atacheza na Ide Mnali katika pambano la raundi nane.