Serikali kupima utendaji wa ma-DC

*Warugenzi nao dawa jikoni WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema Serikali inaandaa vigezo vipya vya kupima utendaji wa Wakuu wa Wilaya ili kuachana na vigezo vya zamani ambavyo havioneshi ufanisi wa kazi zao. Pinda ametoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera mara baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo kutoka …

Dk Bilal ataka mgogoro umalizike bandarini Dar

Na Mwandishi Maalumu Ofisi ya Makamu wa Rais Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya mazungumzo na Chama cha Wakala wa Forodha nchini ili kuondoa mvutano uliopo na hivyo kuimarisha ufanisi katika shughuli za kutoa mizigo bandarini. Dk. Bilal ameyasema hayo jana kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na Mwenyekiti wa chama hicho, …

Mvua zaathiri makazi ya muda ya waathirika Gongo la Mboto

HALI ni mbaya kwa familia zilizoathirika na milipuko ya mabomu kwenye kambi ya Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ), kikosi cha 511 Gongo la Mboto Dar es Salaam na sasa familia hizo zimelazimika kuyakimbia makazi ya muda ya mahema baada ya kujaa maji. Hali hiyo imetokea jana baada ya mvua kubwa kunyesha eneo la Gongo la Mboto na maji kuanza kuingia …

Soko la Big Brother Manzese Dar lavunjwa

Kwa waliowahi kufika Dar es Salaam wanaweza kuwa wanalifahamu soko maarufu la mitumba linaloitwa kwa jina maarufu la Big Brother limevunjwa na sasa wafanyabiashara takribani elfu tatu waliokuwa wakiendesha biashara eneo hilo wanahaha kutafuta eneo lingine. Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU walilazimika kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa mabomu na risasi hewani walipotaka kufunga barabara siku moja baada ya maeneo …

WAZIRI MKUU ASHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO MKOANI KAGERA LEO.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Zamzam kwenye Manispaa ya Bukoba akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera leo. Kushoto ni mkewe Tunu na kulia kwake ni mkuu wa mkoa huo, Mohamed Babu. Picha ya Juu: Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa amevaa kofia aliyozawadiwa na wananchi wa Manispaa ya Bukoba baada ya …

JK ataka bil 54 zilizotoweka kwenye madini zisakwe

Na Mwandishi Maalumu Paris, Ufaransa RAIS Jakaya Kikwete amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuchunguza kiasi cha sh. bilioni 54 ambacho kimebainika kimepotea kutoka katika malipo ya tozo na kodi mbalimbali katika sekta ya madini. Kikwete ametoa maagizo hayo jana mjini hapa alipokuwa akihutubia wajumbe katika Mkutano wa Tano wa Mpango wa Uhamasishaji wa …