MH. KOMBA AMETUMWA BUNGENI AKALALE?

Kwa mpango huu ndugu zangu tutafika? Baadhi ya waheshimiwa wetu wamekuwa ni watu wa kuhudhuria vikao tu, na mara nyingi huwa wanalala wakati vikao vya kujadili maslahi ya nchi vikiendelea. Hilo pozi la Mh. John Komba, ambaye ni mbunge wa Mbinga Magharibi linaonyesha kabisa kwamba amejiweka “comfortable” ili aweze kupata kauisingizi kidogo.

Mwananchi alipukiwa na bomu Lindi

Na Mwandishi Wetu Lindi MKAZI mmoja wa kijiji cha Kitumbikwera mkoani Lindi, Omari Said (29) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu. Tukio hilo limetokea hivi karibuni mjini hapa na majeruhi amelazwa wodi namba sita ambapo ameumia vibaya sehemu ya mgongoni, ubavuni, matakoni pamoja na kukatika kiganja cha …

Wanne wapandishwa kizimbani kwa dawa za kulevya

Na Mwandishi Wetu RAIA wanne wa mataifa tofauti, jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la kula njama na kuingiza dawa za kulevya nchini zenye thamani ya sh bilioni 2.8. washtakiwa hao ambao ni Dennis Okechukwa, Paul Obi ambao ni raia wa Nigeria, mwingine ni raia wa Afrika Kusini, Stani Hycenth pamoja na raia wa nchini …

Kesi ya mwandishi ‘kuomba rushwa’ yaairishwa

Na Mwandishi Wetu KESI inayomkabili mwandishi wa habari ambaye ni mtangazaji wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC1),Jerry Muro na wenzake imeshindwa kuendelea leo kutokana na kutokuwepo kwa wakili wa upande wa mashtaka. Kesi hiyo imetajwa leo Machi 7, 2011 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wao ambapo ilipangwa kusikilizwa …

Dk. Shein: Serikali yangu itafanya mapinduzi ya kilimo

Mwandishi Wetu Pemba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Awamu ya Saba imepanga kufanya Mapinduzi ya Kilimo ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wakulima wadogowadogo hasa hata wale mazao yao yanayoathiriwa na jua la kiangazi. Dk. Shein amesema hayo jana mjini Kengeja Kwajibwa, Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipokuwa akizungumza na …

Dk Shein aanza ziara kuwashukuru Wazanzibari kumchagua

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ameanza kufanya ziara katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar akiwashukuru wananchi kwa kumchagua katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana. Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar tayari juzi amefanya mikutano katika mikoa miwili ya Pemba huku akipangiwa kuendelea katika maeneo mengine. Zifuatazo …