Familia ya Gaddafi yapigwa marufuku Urusi

MOSCOW, Urusi RAIS wa Urusi Dmitry Medvedev juzi alisaini amri ya kumpiga marufuku kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kuingia au kusafiri kupitia eneo la Urusi. Amri hiyo pia imewagusa watu wengine 15 wakiwamo watoto wa Gaddafi na maofisa waandamizi walio karibu naye. Aidha fedha, mali na rasilimali za kiuchumi, ambazo familia ya Gaddafi inazimiliki au kuzidhibiti pia zimetaifishwa. Wiki iliyopita, …

Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi

DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la ‘Babu’, huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi. Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la …

WATANZANIA TUTATOKA VIPI NDANI YA CHUPA?

Karibuni sana ndugu zangu katika ukurasa huu wa Uchambuzi Nyeti! Kama tujuavyo “Msema Pweke Hakosi”, labda tu kwa faida ya wasomaji wetu,   ni wakati muafaka kutumia fursa hii kuwekana sawa. Hii methali ina maanisha kwamba yeyote yule anayesema na nafsi yake huwa hakosei, kwa maana kwamba yale usemayo kwenye nafsi yako ndio yatokeayo. Hivyo basi, cha msingi tunapozungumza na nafsi zetu …

NSSF yajitosa Kiwira

*Yaomba ikabidhiwe mgodi izalishe umeme megawati 500 *Italipa madeni ya bilioni 28/-, mishahara ya watumishi wote *Tanpower kikwazo kwa hisa 70%, wizara yaweka kauzibe *Zito: Mkopo wa kujenga nyumba za Jeshi usitumiwe Kiwira SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejitosa katika mradi mkubwa wa kuzalisha umeme nchini kwa kuonyesha nia ya kununua Mgodi wa Makaa ya Mawe wa …

Maafa ya Japani hayana kifani

WAKATI Japani, taifa lenye nguvu kubwa kiuchumi duniani likihaha katika harakati za uokoaji, mamia kwa mamia ya miili watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi imeendelea kupatikana. Idadi ya vifo kutokana na tetemeko kubwa la ardhi la kipimo cha 8.9 nchini Japani inaweza kufikia 10,000 katika mkoa wa Miyagi pekee. Awali polisi ilisema zaidi ya watu 2,000 wamekufa au hawajulikani …

Umoja wa Kiarabu waunga mkono vikwazo Libya

UMOJA wa Nchi za Kiarabu umeunga mkono wazo la kuzuia ndege kuruka katika anga ya Libya, huku waasi wakiendelea kufurushwa kutoka miji waliyokuwa wakiishikilia. Mkutano maalumu uliofanyika mjini hapa umelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kuweka sera hiyo hadi mgogoro wa sasa utakapomalizika. Uingereza na Ufaransa ziliunga mkono wazo hilo lakini hazikuungwa mkono vya kutosha na Umoja …