Loliondo sasa ni janga

*Wastani wa watu 15 wafia kwenye foleni kila siku *Ugonjwa wa kuhara damu waibuka kwa kasi kubwa *Ofisa Kilimo Wilaya ya Misungwi afia kwenye foleni *Zahanati haina dawa, wahudumu, glovu, vitanda *Wanajeshi kutoka Kenya wafika kijijini Samunge kwamba wastani wa watu 15 wanafia kwenye foleni na wengine miili yao kuharibikia ndani ya magari. Maelfu kwa maelfu ya watu wamekwama kwenye …

Ni huzuni nchini

Baadhi ya Wanamuziki wa Kundi la 5 Star waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea juzi maeneo ya Mikumi Morogoro, wakiwa kwenye Ukumbi wa Ikweta Gril, baada ya kuwasili wakitokea Hospitali ya Morogoro jana. Picha na Mpigapicha Wetu NI HUZUNI, ndivyo unavyoweza kuzungumzia ajali mbaya iliyochukua maisha ya wanamuziki 13 wa kundi la taarabu la Five Stars. Ajali hiyo mbaya na pengine kubwa …

NANI BADO HAJAENDA KUMUONA ‘BABU’ LOLIONDO?

  Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapile akimpa dawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) William Lukuvi na Rosemary Nyerere baada ya Lukuvi kumaliza kuukagua mti unaozalisha dawa hiyo. Lukuvi alitua Loliondo mwishoni mwa wiki iliyopita. Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Masapile kunywa dawa  wakiagana na Mchungaji na kumtakia kheri baada ya kupata kikombe.Kulia …

CUF YASISITIZA MAANDAMANO YA CHADEMA NI UCHOCHEZI

Na Mwandishi wetu, Tanga. CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewaasa watanzania kuepuka kushiriki maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa ni ya uchochezi yenye lengo la kuliingiza taifa katika machafuko. Pia kimeitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutofumbia macho kauli za uchochezi dhidi yake. Hata hivyo, CUF imesema kinachofanywa na viongozi wa Chadema kwa kuhamasisha wananchi kutoiamini serikali iliyopo …

Chadema ngangari

Chasisitiza kuendeleza maandamano Chasema ni uamuzi wa Kamati Kuu Chasema si ya kuiangusha serikali Na Khamis Mkotya CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza kuwa kitaendeleza maandamano ya amani nchi nzima. Kimesema kitafanya hivyo licha ya viongozi wa Serikali kulalamikia maandamano ya chama hicho yaliyofanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa hivi karibuni. Uamuzi huo ni agizo la Kamati Kuu …

Libya yashambuliwa kutoka kila kona

UINGEREZA, Marekani na Ufaransa zimeyashambulia majeshi ya kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi kutokea angani, majini na nchi kavu katika tukio la kwanza la utekelezaji amri ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kuzuia ndege kuruka. Maofisa wa Pentagon, wizara ya ulinzi ya Marekani wanasema Marekani na Uingereza zimevurumisha zaidi ya makombora 110 huku ndege za Ufaransa zikiyashambulia majeshi yanayomtii Gaddafi …