Mtuhumiwa wa uhujumu uchumi amkataa hakimu

  NA Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na Fedha, Grace Martin, wamewasilisha ombi la kumkataa hakimu anayesikiliza kesi yao ya uhujumu uchumi ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 2. Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana washitakiwa hao walitakiwa kuanza kujitetea, lakini kabla ya jambo …

CCM waijibu Chadema, watoa kauli nzito

Na Mwandishi Wetu CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimejibu hoja zilizoelekezwa kwao na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichomalizika hivi karibuni. Wakijibu hoja hizo, CCM imesema kwamba isingependa kufanya majibizano na CHADEMA kwa kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wana kazi nyingi za kufanya kutekeleza ilani ya chama ilhali CHADEMA …

Sumatra wajipanga kuwajibu matrafiki

Na Joachim Mushi SAKATA la malalamiko yaliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) dhidi ya baadhi ya askari polisi rafiki kuwa ndio wamiliki wa magari mabovu na yasiofuata taratibu katika sekta ya usafirishaji abiria, limeingia sura mpya baada ya SUMATRA kudai wanajipanga kutoa tamko. Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano wa SUMATRA, …

Roho za Watanzania zaendelea kuteketea

BREAKING NEWZZZ Roho za Watanzania zaendelea kuteketea *Ajali mbaya yaua tena 9, yajeruhi wengine Na Joachim Mushi IKIWA ni siku chache tangu ajali ya wasanii wa kundi la five star kutokea Mkoa wa Morogoro na kuua wasanii 13 wa kundi hilo na nyingine kutokea tena eneo jirani na lile na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa, imetokea nyingine mbaya na …

ABDALLAH SALUM: Mzee aliyekatwa uume kwa deni la Sh 150,000

AMINI usiamini, tukio hili limetokea hivi majuzi. Wiki iliyopita nilikuwa katika ziara ya kikazi katika Jimbo la Kisarawe nikiwa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo, Seleman Jafo. Tulitembelea vijiji vingi vikiwamo Sungwi, Masaki, Chang’ombe, Mfuru, Kikwete, Boga, Msanga, Chole na Kijiji cha Kibuta. Tukiwa katika Kijiji cha Kibuta, tuliambiwa kijijini hapo mmoja wa wapiga kura wa mbunge huyo aliyefahamika kwa …