Mbunge atoa ushuhuda wa Loliondo kikaoni

Na Mwandishi Wetu Kilindi MBUNGE wa Jimbo la Kilindi, Beatrice Shelukindo, amesema kuponya kwa tiba ya kikombe cha dawa inayotolewa na Mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapila ‘Babu’ wa kijiji cha Samunge, kunatokana na imani ya mgonjwa. Mbunge Shelukindo aliyasema hayo juzi mjini hapa alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya shughuli za mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi 2011/12 katika kikao cha …

Babu Loliondo ashindwa ‘waponya’ wenye VVU

Na Mwandishi Wetu Kahama WANANCHI wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo Ukimwi wameshauriwa kuendelea kutumia dawa wanazopewa na wataalamu hospitalini hata kama wamefanikiwa kunywa kikombe cha dawa ya Mchungaji Ambilikile Mwasapila. Ushauri huo ulitolewa jana mjini hapa na Meneja wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali (SHIDEPHA+), Venance Muzuka linalojishughulisha na kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwa na watoto yatima pamoja na …

CWT Kilimanjaro wamlaani RC

Na Mwandishi Wetu Moshi CHAMA cha Walimu (CWT) mkoani Kilimanjaro wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Kalembo cha kuiamuru Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huu kumkamata Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Moshi Vijijini, Hubert Mariki alipokuwa akitekeleza majukumu yake ya kudai haki za wanachama wake. Katika tamko lao lililotolewa …

Slaa awalipua Malecela, Mangula, Magufuli

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa amekoleza moto wa vita ya ufisadi kwa kuibua tuhuma mpya dhidi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Waliotajwa wapya ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), John Malecela, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Dk. Slaa alitoa orodha hiyo …

JAMBO LEO MABINGWA NSSF CUP

TIMU ya soka ya Jambo Leo ‘Wagumu Star’ inayomilikiwa na kampuni ya Jambo Concepts Ltd, imetwaa Ubingwa wa Kombe la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuifunga timu ya NSSF katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Sigara Chang’ombe Dar es Salaam. Katika mchezo huo mkali uliofanyika jana, timu ya NSSF ndio walio kuwa wa …

Babu wa Loliondo awashukia wanaomuiga

Ngorongoro MCHUNGAJI mstaafu Ambilikile Mwasapila (Babu) amesema baadhi ya watu wanaodai kutibu kwa kutumia tiba ya kikombe kama anavyofanya yeye ni wauaji, wezi na wanasumbuliwa na njaa, hivyo amewataka wananchi wawapuuze. Akizungumza na waandishi wa habari kutoka Jijini Mwanza, Aprili 13 mwaka huu, Mwasapile alisema watu walioibuka baada ya yeye kuanza kutoa huduma ya tiba ya kikombe wanasumbuliwa na njaa …