Katibu wa Bunge awaponda wabunge

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Thomas Kashililah amesema wabunge wengi kutofahamu vema kanuni za uendeshaji wa Bunge, ndiyo chanzo cha mivutano na vijembe kutawala vikao vya Bunge la 10. Kashililah alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hali hiyo pia inachangiwa na uwepo wa …

Dk Shein kutembelea Uturuki

Na Rajab Mkasaba RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuondoka nchini Aprili 28 kuelekea Jamhuri ya Uturuki kwa ziara ya mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Abdullah Gul. Katika ziara hiyo, Dk. Shein atafuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Nchi Ofisi ya …

Irani yatoa USD mil 1.2 kusaidia Kilimo Kwanza

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Irani imepanga kutoa dola za kimarekani milioni 1.2 (dola milioni 1.2) kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa vitendo kampeni za Kilimo Kwanza. Taarifa imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Balozi Msaidizi wa Iran nchini Tanzania Bahman Ahmadi alipotembelea Wizara ya Viwanda na Biashara na kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu. Katika mazungumzo …

JK aongoza maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano

Na Beatrice Mlyansi na Joseph Ishengoma, Maelezo-Zanzibar RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete amewaongoza watanzania kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kitaifa Zanzibar. Sherehe hizo zilifanyika jana Uwanja wa Amaan Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Rais alipigiwa mizinga …

Ajali nyingine yaua wanane Rukwa

Na Mwandishi Wetu Sumbawanga WATU wanane wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia mkesha wa Pasaka kwenye Milima ya Lyamba Lyamfipa ulipo mpakani mwa wilaya za Mpanda na Nkasi mkoani Rukwa. Kwa mujibu taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa …