Sekondari za kata zipo kisiasa zaidi

Na Joachim Mushi HATUA ya Serikali kuamua kujikita kutatua upungufu wa shule za sekondari nchini ni nzuri. Nasema ni nzuri kwa kuwa hivi sasa kuna idadi kubwa ya shule hizo ambazo zinajulikana maarufu kama sekondari za kata. Ni kweli kwamba hata nafasi za wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Niseme wazi kwamba kama kweli shule hizi …

Shule za Serikali zapeta Kidato cha Sita

SHULE za Sekondari za Serikali zimeng’ara katika matokeo ya Kidato cha sita mwaka 2011 baada ya wanafunzi wake saba kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi kumi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ni wavulana.Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako aliwataja wanafunzi …

Dk Shein awasili nchini Uturuki kwa ziara

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania, Dk. Sander Gurbuz, (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ankara nchini Uturuki, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo.

Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’ Dar

Wasanii mbalimbali na vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’, wakicheza staili moja kwa pamoja wakati wa Tamasha hilo lililofanyika juzi kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam, Tamasha hilo likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha liliandaliwa na kampuni ya simu …

Mwalimu acharaza viboko 100 wanafunzi

WAKATI Serikali ikijaribu kupunguza adhabu za viboko kwa wanafunzi na kuweka mwongozo na utaratibu wa adhabu hizo, wananfunzi wanne wa Shule ya Sekondari Nsoho mkoani Mbeya wamejeruhiwa baada ya kuchapwa viboko 100 kila mmoja. Tukio hilo linadaiwa kufanywa April 22 mwaka huu na mwalimu Lukindo Mwakanyasi,ambaye anafundisha shuleni hapo kwa mkataba. Wakizungumza hivi karibuni kwa masharti ya kutotajwa majina, baadhi …

JK amteua Mshana kushika nafasi ya Tido TBC

RAIS JAKAYA KIKWETE JANA ALIMTEUA ALIEKUWA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI-MAELEZO, CLEMENT MSHANA KUWA MKURUGENZI MPYA WA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (TBC) KUZIBA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA MKURUGENZI ALIEMALIZA MUDA WAKE, TIDO MHANDO.UTEUZI HUO UMEFANYWA LEO NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE.