Mwalimu aweka poni nyaraka za shule kwa pombe

Mwandishi Wetu Sumbawanga MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Chipu, Kata ya Kasense Manispaa ya Sumbawanga aweka poni Muhtasari wa masomo 13 kwa mfanyabiashara wa pombe na vinywaji baridi kwa ajili ya kuaminiwa na kisha kukopeshwa bidhaa hiyo. Tuhuma hizo zimetolewa jana na mfanyabiashara maarufu, Singo Nzinyangwa anayemiliki duka la ‘Zawadi Store’ lililopo Manispaa ya Sumbawanga mjini. Amesema mwalimu huyo …

Kikwete awataka mawaziri waache ubabe, dhuluma, uzinzi

Na Said Mwishehe Dodoma RAIS Jakaya Kikwete amewataka mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na manaibu wao katika Serikali yake kutotumia nafasi zao vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya dhuluma, wizi, ulevi, uzinzi, ubabe na udhalilishaji. Amewataka watambue kuwa, hakuwateua kushika nafasi hizo kwa ajili ya kujifungua ofisini na kutazama TV, kusoma magazeti na kutumia muda mwingi kuangalia mtandao; bali kwa …

Benki, asasi za fedha ondoeni masharti magumu-Wajasiriamali

Na Mwandishi Wetu Moshi BENKI na asasi mbalimbali zinazojihusisha na kutoa mikopo zimetakiwa kulegeza masharti ya mikopo hiyo ili kuwawezesha wajasiriamali wengi kupata huduma hiyo kirahisi na hivyo kuongeza mitaji yao, tofauti na ilivyo sasa. Wito huo umetolewa juzi mjini hapa na Waziri wa viwanda, Biashara na Masoko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami …

‘Siasa zisiingizwe kwenye shughuli za maendeleo’

Na Anna Nkinda, Maelezo Mkuranga WANANCHI wilayani Mkuranga wametakiwa kuachana na itikadi za kisiasa katika shughuli za maendeleo, kwani suala la maendeleo linamgusa kila mwananchi bila kujali itikadi za kisiasa. Wito huo umetolewa jana mjini hapa na mke wa Rais, Salma Kikwete wakati akifungua Chama Cha kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS) kitakachojulikana kama ‘Salma Kikwete’ kilichopo kijiji cha Hoyoyo Mkoa …

KIFO CHA OSAMA:NDIO HATMA YA DONALD TRUMP KISIASA?

Nilipokiona hichi kikaragosi cha ndugu yetu GADO, niliguswa sana na nikaona sina budi kuandika mawili matatu hapa katika baraza letu la uchambuzi nyeti.  Tajiri la vitega uchumi wa majumba Marekani, Bw. Donald Trump ameumbuka hivi karibuni kutokana na ile hulka yake ya kudadisi na kutilia mashaka uraia wa Rais Obama. Siku za hivi karibuni, Trump amekuwa mstari wa mbele kuwahimiza …