Nahodha azungumzia Wazenji kuchoma mabanda ya Wabara

Na Said Mwishehe Dodoma WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha amesema kubomolewa kwa mabanda 73 ya wafanyabiashara mjini Unguja Zanzibar ni uvunjifu wa sheria hivyo atahakikisha sheria kali zinachukua dhidi ya watakaohusika. Nahodha amesema haamini kama tukio hilo lina uhusiano na mambo ya kisiasa ama ubaguzi, hivyo kuomba viachiwe vyombo vya sheria ili viweze kutekeleza majukumu …

Dk Bilal azitaka nchi tajiri kutimiza ahadi

Na Mwandishi Maalum Instabul TANZANIA imetoa wito kwa nchi tajiri kutambua nafasi yao katika kuzikwamua nchi masikini ili ziweze kukuza uchumi wake na kuwasaidia wananchi waliomo katika nchi hizo. Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akihutubia mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa unaojadili maendeleo ya nchi masikini nchini …

CCM yagawanyika Songea

CCM yagawanyika Songea Na Mwandishi Wetu Songea WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatengeneza mazingira ya kujisafisha kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye matawi kwa kauli ya kujivua gamba, baadhi ya wanachama Wilaya ya Songea Vijijini wameushutumu uongozi wao kuanza kukigawa chama hicho. Baadhi ya wanachama hao wamelilalamikia kundi la viongozi wilayani humo kwa kitendo cha kumtelekeza Mwenyekiti wa CCM Wilaya …

Mashindano ya KCB East African Tour 2011 yazinduliwa

Na Janeth Mushi Arusha MASHINDANO ya Benki ya Biashara Kenya (KCB) East Africa Golf Tour 2011 yanayoanza leo mjini hapa katika viwanja vya Arusha Gymkana Club, mshindi wa mashindano hayo anatarajia kujinyakulia kitita cha sh. 3,630,000 fedha za Kitanzania. Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi …

Madiwani walilia mishahara kama wabunge

Na Mwandishi Wetu Kilwa MADIWANI wa halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Lindi wameishauri Serikali kubadili mfumo wa malipo kwa viongozi hao kutoka kulipwa posho na kuanza kulipwa mishahara ili nao waweze kukopeshwa katika taasisi za fedha, kama ilivyo kwa watumishi wengine. Ombi hilo limetolewa juzi na madiwani hao kwenye mkutano wa Jumuia ya Tawala za Mitaa (ALAT), tawi la Lindi …