Mawakala Morogoro kuishtaki Serikali

Na Mwandishi Wetu Morogoro MAWAKALA wa pembejeo wanakusudia kuiburuza mahakamani Serikali mkoani Morogoro kwa kile kushindwa kulipa deni la zaidi ya sh. bilioni 3, gharama ambazo zilitumiwa na mawakala hao kusambaza pembejeo msimu wa kilimo wa 2009/10 na 2011/12. Hatua hilo imepitishwa juzi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mawakala hao kilichokaa kutafuta ufumbuzi wa madeni ambayo wamekuwa wakiidai …

Warusi waonesha nia kuwekeza Tanzania

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Shaaban Mwinjaka amewataka wawekezaji wenye nia njema kuja nchini na kushirikiana na wazalendo katika kutumia fursa mbali mbali zilizopo nchini kwa faida na maendeleo ya pande zote mbili. Dkt Mwinjaka ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo mafupi kati yake na ujumbe wa wawekezaji kutoka nchini Urusi wenye nia …

Waziri wa Nchi azungumza na Balozi wa Iran

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya Huvisa akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania, Mohsin Movahhed kuhusu Masuala ya Kuanzisha Mashirikiano baina ya Tanzania na Iran kwenye Mauala ya Mazingira (Picha na Ali Meja)

Waziri Mkuu wa India kuja Tanzania

TAARIFA KWA MHARIRI Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Manmohan Singh amekubali mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutembelea Tanzania wiki ijayo. Mheshimiwa Singh amekubali mwaliko huo katika barua yake aliyomwandikia Rais Kikwete na iliyokabidhiwa kwake na Balozi wa India katika Tanzania, Mheshimiwa K.V. Bhagirah wakati Balozi huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais …

Taratibu za kuvuna Sao Hill zawekwa wazi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII TAARIFA KWA UMMA TARATIBU ZINAZOFUATWA KATIKA UVUNAJI WA MAZAO YA MISITU KWENYE SHAMBA LA SAO HILL Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazofuatwa katika uvunaji wa mazao ya misitu katika shamba la miti la Saohill. Baadhi ya magazeti ya tarehe 19 Mei 2011 yaliandika kuhusu uvunaji wa …

Leo ni mwisho wa dunia

CALIFORNIA, Marekani MWISHO wa dunia umefika na huenda tusiione tena Jumapili ya kesho kwani dunia inafikia mwisho wake leo Jumamosi, kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa moja la California. Mchungaji Harold Camping wa California, ametabiri kuwa mwisho wa dunia ni leo Mei 21 mwaka huu saa moja kamili usiku. Mchungaji Camping kwa kutumia mahesabu ya tarehe na mafunzo ya Biblia, …