IGP Mwema awapa changamoto Sumatra, trafiki

Na Mwandishi wetu Morogoro INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema amewataka watendaji wake kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) kubuni njia za kitaalamu kuthibiti ama kupunguza matukio ya ajali za barabarani nchini. Inspekta Mwema alitoa tamko hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga mkutano wa pamoja kati ya watendaji wa SUMATRA na …

Wamisri kuchezesha Simba v WYDAD

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco litakalofanyika Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri. Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za …

KWA PICHA HII: WAZIRI MKUU WA INDIA NI MFUASI WA CHADEMA?

Mh Dr. Manmohan Singh, ambaye ni waziri mkuu wa India anatarajiwa kutua Bongo muda si mrefu (Tafadhali, rejea taarifa yetu ya awali)  kwa shughuli maalum. Nilipoona picha hii nikastuka kidogo, na kujiuliza itakuwa aje siku ya kutua Bongo halafu anarudia ishara yake ya vidole viwili kama tuonavyo hapo kwenye picha? Nafikiri itakuwa kama Waingereza wasemavyo “Very Interesting!”  Wewe unaona imekaa vipi hii?

Rais Kikwete ahani msiba wa Shekh Yahya Hussein

Rais Kikwete akipokewa na Hassan Yahya Hussein, Mtoto mkubwa wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein alipokwenda kuhani msiba wa mnajimu huyo maarufuf nyumbani kwa Marehemu Magomeni Mwembe chai Mei 22

JK akiwa kwenye msiba wa Hassan Mwinyimvua

Rais Kikwete akiwa na ndugu, jamaa na marafiki aliokwenda kuhani msiba wa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM, marehemu Athumani Hassan Mwinyimvua mtaa wa Matombo Magomeni Mwembe Chai Mei 22

TAWLA kusaidia wanawake, watoto kisheria

Na Tiganya Vincent, MAELEZO-Dar es Salam Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kimeahidi kuendelea kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto wengi wanaokandamizwa pindi wanapokuwakidai haki zao za msingi ili kujenga jamii inayozingatia haki na usawa kwa jamii yote. Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa TAWLA Marie Kashonda wakati akiongea na waandishi wa habari …