Ofisi ya Mwanasheria iheshimu kanuni-Waziri Kombani

Na Ismail Ngayonga MAELEZO, Dar es Salaam WAFANYAKAZI katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wametakiwa kuheshimu kanuni za fedha na kuweka sawa hesabu ili kutekeleza mikakati anuai iliyopo kiufasaha na ukamilifu. Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali uliofanyika katika …

Baba mahakamani kwa kutaka kuuwa kichanga

Na Mwandishi Wetu Maswa POLISI wilayani Maswa, Mkoa wa Shinyanga imemfikisha mahakamani, Baya Mlyagape (24) mkazi wa Kijiji cha Songambele Kata ya Ipililo kwa kosa la kutaka kumua mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitano. Akisomewa mashitaka mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Maswa, Thomson Mtani; ilielezwa kuwa mshitakiwa alitenda unyama huo Mei 5, 2011 majira ya saa nne usiku …

Wafungwa wa kesi za EPA wakielekea gerezani

Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein na binamu yake Rajabu Maranda wakiwa katika ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ndani ya gari wakati wakitoka Mahakamani kupelekwa gerezani baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela.

Watuhumiwa wa EPA wawili waenda jela miaka 5

Na Mwandishi Wetu WATUHUMIWA Farijala Hussein na binamu yake Rajabu Maranda wa kesi ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano. Maranda ambaye ni mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na mpwa wake, Hussein walihukumiwa kifungo hicho jana jijini Dar es Salaam katika Mahakama …

239,250 wanywa dawa za mabusha, matende

Na Mwandishi Wetu Morogoro SHUGHULI za uhamasishaji wa wananchi kunywa dawa za ugonjwa wa usubi, matende na mabusha Wilaya ya Morogoro zimekuwa na mwitikio mzuri baada ya wananchi 239,250 kujitokeza na kupatiwa dawa hizo. Kwa mujibu wa taarifa za Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Debora Kabudi iliyotolewa mwishoni mwa wiki mjini hapa, watu 239,250 waliojitokeza katika tukio hilo wamepatiwa …

Dk Mahanga asaidia vicoba Kimanga D’Salaam

MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga akikabidhi sh. 500,000 kwa umoja wa VICOBA katika Mtaa Tembomgwaza Kata ya Kimanga, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa umoja huo unaojumuisha vikundi 10 juzi.