BONGO MOVIE STARS FC YATUA MWANZA

Steve Nyerere ‘Messi’ na JB wakiingia uwanja wa Kirumba taratiiiiibu tayari kupambana na timu ya waandishi wa habari wa Mwanza ijulikanayo kama Rock City Stars katika mchezo wa hisani kuchangia ununuzi wa madawati kwa ajili ya shule ya msingi ya Ilemela, ambapo matokeo yalikuwa 1-1. (Picha na John Bukuku)

Ajali; Wawili wafa 28 wajeruhiwa Iringa

Francis Godwin Iringa WATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 28 kujeruhiwa vibaya baada ya fuso lenye namba za usajili T115 ANZ walilokuwa wakisafiria kwenda Mnadani Pawaga Iringa kupinduka. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1 asubuhi leo katika Milima ya umasaini barabara kuu ya Iringa -Pawaga wakati wafanyabiashara hao zaidi ya 50 wakielekea mnadani huku chanzo cha ajali hiyo …

TANZANIA YATESA MAREKANI!

  Na Rungwe Jr. California, USA Mwisho wa Juma lililopita nilikuwa Santa Barbara, California, moja kati ya miji mizuri sio tu Marekani, bali duniani kwa ujumla. Baada ya uchovu wa kuzunguka hapa na pale, nikaamua kuingia kwenye Mgahawa maarufu wa ‘Starbuck’ ili kupata kikombe cha kahawa!(Sio kikombe cha Babu!) Nilipoingia tu ndani ya Mgahawa nilikaribishwa na picha hii ya mnyama Tembo na juu yake chapisho kubwa la …

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kufunguliwa kwa mkutano wao mkuu. Watatu kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani akifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema na watano kutoka kulia ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju. (Picha …

Ruvuma ‘out’ Kili Taifa Cup

Na Asha Kigundula, Arusha TIMU ya soka ya Mkoa wa Ruvuma jana imeaga mashindano ya Kili Taifa Cup baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-2 toka kwa timu ya Mkoa wa Mbeya Mapinduzi (Stars) mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini hapa. Dakika ya 3 ya mchezo Gaudence Mwaikimba aliipatia Mbeya goli la kwanza kwa kupiga mpira …

Nani kucheza fainali kati ya Ilala na Mwanza?

Na Asha Kigundula Arusha TIMU ya soka ya Mkoa wa Ilala leo itakuwa na kibarua kigumu itakapovaana na timu ya soka ya Mkoa wa Mwanza katika hatua ya Nusu fainali ya michuno ya Kili Taifa Cup inayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani hapa. Kindumbwendumbwe hicho kitaanza saa 10.00 Alasiri ambapo mshindi wa mchezo huo atamsumbili mshindi wa michezo …