Mchujo wa kwanza U23 Tanzania na Nigeria Juni 5

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Boniface Wambura, Ofisa Habari wa TFF Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itachezwa Juni 5 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Tumepanga muda huo kwa vile …

Simba wakatiliwa kuwatumia Samata na Ochan

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Boniface Wambura, Ofisa Habari wa TFF Wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan ambao Simba ilitaka kuwatumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco hawana uhalali wa kuchezea timu hiyo. Simba kupitia TFF ilitaka kufahamu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kama inaweza kuwatumia wachezaji hao kwa …

Dk Bilal akagua miradi ya maendeleo Kaskazini Unguja

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akioneshwa sehemu ya madawati yaliyotolewa msaada na wafadhili wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, wakati alipofika katika shule ya Sekondari Nungwi kuzindua vyumba saba vya madarasa, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali mkoa wa Kaskazini Unguja, Mei 22, 2011. (Picha na Muhidin Sufiani …

JK ashiriki mazishi ya mke wa George Kahama

Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Mary Kahama Mke wa Waziri mstaafu na Mwanasiasa mkongwe Clement George Kahama (aliyesimama nyuma kulia) wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana jioni (Picha na Freddy Maro)

Ajali mbaya Iringa

Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T115 ANZ likiwa limepinduka na mizigo kuzagaa baada ya kupata ajali mkoani Iringa jana. Katika ajali hiyo watu wawili walikufa na wengine 28 kujeruhiwa vibaya. (Picha na Francis Godwin, Iringa)