JK akiwa Addis Ababa mkutano wa AU

Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme Mswati III wa Swaziland wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Mai 25, 2011. (Picha kwa hisani ya Ikulu)

Viongozi G8 kukutana leo Ufaransa

Viongozi wa dunia wanatarajiwa kukutana katika eneo Deauville nchini Ufaransa, kwenye kongamano la mataifa manane yenye utajiri mkubwa zaidi duniani G8. Mkutano wa leo unatokea wakati kumeibuka mataifa mengine ambayo uchumi wake unakua kwa kasi na kuibua hoja ya ushawishi na umuhimu wa G8. Hata hivyo wadadisi wamesema matuko ya hivi karibuni hususan harakati za mageuzi ya kidemokrasia katika nchi …

Dk. Shein akiwa Jimbo la Makunduchi

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame, baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Tangi la Maji la, Jimbo la Makunduchi, huko Kizimkazi Mkunguni jana, akiwa katika ziara wilaya ya kusini Unguja.

CHADEMA YATOA TAARIFA KUHUSU UCHAGUZI WA ‘BAVICHA’ TAIFA

  Taarifa inatolewa kwa umma kuhusu orodha ya wagombea waliorudisha fomu na utaratibu wa uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ngazi ya taifa kama ifuatavyo ORODHA YA WALIORUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA: Nafasi ya Mwenyekiti (Wagombea 10)- Aidan Sadik P., Benard A. Mao, Benard Saanane, Deogratias Kisandu, Edwin Soko, Greyson Nyakarungu, Habib Mchange, John Heche, Masood S. Suleiman na …

Ziara ya Dk. Shein Mkoa wa Kusini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Uendeshaji wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Bibi Asha Khalfan, alipoangalia bidhaa za vikundi vya ushirika katika mkutano wa watendaji wa Mkoa wa Kusini Unguja, katika mkutano wa majumuisho ya Ziara aliyoifanya katika Mkoa huo, huko Chuo Kikuu cha …

Dk Shein: Changamoto za wananchi zitapatiwa ufumbuzi

Na Mwandishi Wetu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa miongoni mwa vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ni kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta za maji, umeme na huduma nyengine za kijamii zinapatiwa ufumbuzi haraka. Dk. Shein aliyasema hayo jana mjini hapa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na wakulima …