Madiwani Dodoma wataka kujiondoa NHIF

Na Joyce Kassiki Dodoma BAADHI ya madiwani wa Halmashauri ya Kongwa wametishia kujiondoa kwenye mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa baada ya kutoridhishwa na utaratibu uliowekwa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).  Wakizungumza kwenye semina kabla ya kuanza kwa kikao cha madiwani katika Halmashauri hiyo, madiwani hao walidai utaratibu wa mfuko huo ni mgumu kutokana na kutoza fedha …

Mahakama yaamuru Mbowe, Dk Slaa, Ndesamburo wakamatwe

Na Janeth Mushi Arusha MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imetoa amri ya kukamatwa kwa watuhumiwa nane (8) pamoja na wadhamini wao, wakiwemo Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe na Dk. Willbrod Slaa kisha kufikishwa mahakamani hapo wakati wowote. Viongozi wengine ambao nao wanatakiwa kukamatwa ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo …

Waliotafuna fedha za miradi wamtisha maisha DC

Na Mwandishi Wetu Bagamoyo MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Magesa Mulongo, ameanza kupata vitisho kutoka kwa baadhi ya watumishi ambao ameagiza wakatwe mishahara kufidia fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimeliwa chini ya usimamizi wao. Mkuu huyo alisema hayo jana mjini hapa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, na kuomba kamati hiyo isaidie ili walio kula …

Mwaka wa kimataifa wa Kemia

Na Maulid Kapolo WAZIRI wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Profesa Makame Mbarawa amewataka walimu, wazazi pamoja na jamii kwa ujumla kuwahamasisha na kuwashawishi wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kupenda masomo ya sayansi hususani kemia. Taarifa hiyo ilitolewa jana, Dar es Salaam na Profesa Mbarawa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya masomo ya sayansi nchini katika uzinduzi wa …

CCM Kibaha yawacharukia watendaji

  Na Mwandishi Wetu Kibaha CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini kimewacharukia watendaji wa ngazi mbalimbali katika halmashauri ya mji huo kutokana na baadhi yao kutotekeleza majukumu yao ipasavyo. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Maulid Bundala kwenye kikao cha madiwani kilichofanyika juzi mjini hapa, ambapo alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakiwashutumu watendaji …

Wabunge wawaadhibu wakuu wa idara Kisarawe

Na Mwandishi Wetu Kisarawe KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LACC), juzi imewapa wakuu wa idara anuai za Kisarawe adhabu ya kukatwa mishahara yao ya mwezi ujao kutokana na kile kutoa taarifa za uongo katika miradi ya maendeleo za mwaka 2008/09. Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Idd Azan, alipokuwa akitoa taarifa za ukaguzi za …