Simba yachwapwa 3-0 na WYDAD

TIMU ya Simba ya Msimbazi jijini Dar es Salaam imeshindwa kuwapa raha mashabiki wake baada na Watanzania kwa ujumla baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya WYDAD ya Casablanca nchini Morocco. WYDAD ilianza kuharibu furaha ya mashabiki wa simba katika dakika ya 88 ilipoandika bao la kwanza na 89 bao la pili na kukandamiza bao la tatu tena …

Siku Deogratius Temba alipofunga ndoa na Sylivia

MAI 21, 2011 itabaki kuwa kumbukumbu ya milele kwa mwanahabari Deogratius Temba mkewe Sylvia Rwanyamva baada ya kufunga pingu za maisha. Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofayika katika Ukumbi wa King Palace Sinza Kamanyora. Picha mbalimbali  ni Deogratius Temba akiwa na mkewe Sylvia katika pozi eneo la Mlimani City jijini …

Basi la Sumry laua 13 kwenye ajali Mbeya

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya AJALI mbaya ya basi la kampuni ya Sumry lililokuwa linatoa huduma ya usafiri kutoka Arusha kuelekea mkoani Mbeya iliyotokea eneo la Igawa mpakani mwa Mbeya na Iringa imeua watanzania 13 papo hapo na wengine watatu kufia katika hospitali ya wilaya ya Mbarali na wengine 9 kujeruhiwa miili yao. Ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo aina …

PINDA: TUNAHITAJI KUBAINI KILIMO CHA UMWAGILIAJI KINACHOTUFAA

Na Irene Bwire WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kilimo cha umwagiliaji kitainua uzalishaji wa chakula nchini lakini inabidi Serikali ijipange kubaini ni aina gani ya teknolojia inahitajika katika kilimo hicho. Ametoa kauli hiyo Mei 27, 2011 akizungumza na ujumbe wa kampuni ya Jain Irrigation Systems Ltd kutoka India, alipokutana nao ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo ina …

Mke wa Waziri Mkuu India aipa WAMA mil. 15

Na Anna Nkinda – Maelezo MKE wa Waziri Mkuu wa India, Mama Gursharan Kaur ametoa msaada wa sh. milioni 15 kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleoo (WAMA) fedha ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali za kuwasaidia watanzania zinazofanywa na taasisi hiyo. Msaada huo umetolewa leo katika ofisi za WAMA zilizopo jijini Dar es Salaam wakati mama Kaur alipoitembelea taasisi hiyo inayoongozwa …

India yaahidi kuisaidia Tanzania teknolojia

Na Joseph Ishengoma – MAELEZO SERIKALI ya India imeahidi kuisaidia Tanzania katika nyanja ya teknolojia ili kuongeza uzalishaji katika mazao ya kilimo. aidha, India imekubali kusaidia uimarishaji wa viwanda vidogo vidogo na kutoa mafunzo ya kitabibu kwa watanzania hasa katika magonjwa ya moyo, kansa na figo. Rais Jakaya Kikwete amewaambia waandishi wa habari Ikulu jijini Dar Es Salaam kuhusu makubaliano …