Utapeli waendelea kwa ‘Babu’ Loliondo

    Na Janeth Mushi,  Thehabari  Arusha  SERIKALI mkoani hapa imetoa onyo kali kwa baadhi ya watu  wanaoghushi mihuri ya vibali vya magari yanayopeleka wagonjwa kijijini Samunge kwa Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila  na kuviuza kinyume cha kanuni na sheria. Onyo hilo limetolewa leo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kufuatia …

Polisi waamriwa kumsaka Mbowe na kumkamata

Na Janeth Mushi, Arusha HAKIMU mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Charles Magesa amemuamuru Ofisa wa Kituo Cha Polisi mkoani hapa kutekeleza amri ya Mahakama ya kumkamata Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kwa kushindwa kutii amri ya Mahakama. Hakimu Magesa ametoa agizo hilo leo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi …

Wasichana wakamatwa wapimwa bikra Misri

Shirika la kutetea haki za binaadam la Amnesty International limeitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi kamili baada ya maofisa wa juu wa kijeshi kukiri kuwa waliwafanyia vipimo vya ubikira, wanawake waliokuwa wakiandamana hivi karibuni. Pamoja na hayo, Amnesty imetaka wote waliohusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu udhalilishaji huo. Tuhuma hizo ambazo zinadaiwa kutokea kwa wanawake waliokuwa wakiandamana baada …

Oxfam yaja na kampeni mpya ya ‘otesha’

OTESHA ni kampeni mpya ya Oxfam ya juu ya njia bora za kuotesha, kugawana na kuishi pamoja. Ni kampeni yetu sote, mabilioni ya watu tunaokula chakula na zaidi ya wenzetu bilioni moja wanawake na wanaume wanaozalisha chakula hicho. Ni kampeni yenye kutafuta suluhisho kwa mustakabali bora wenye uhakika wa chakula kwa kila binadamu. Hivi karibuni idadi ya watu itafikia bilioni …

Mrwanda, Kassim waitwa stars, wazuiliwa kuja

WACHEZAJI Dan Mrwanda na Abdi Kassim ni miongoni mwa wachezaji saba wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi walioitwa na kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen lakini tayari timu zao zimekaa kuwaruhusu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura amesema wachezaji hao waliitwa kwa ajili ya mechi ya Taifa Stars dhidi …

TFF yataja viingilio Nigeria Vs Tanzania U 23

Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itafanyika Jumapili (Juni 5, 2011) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili jioni.   Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 1,000 kwa viti vya kijani, bluu na rangi ya chungwa …