Breaking News, Chadema wapigwa mabomu Dar

Na Joachim Mushi, Thehabari, Dar es Salaam TAIFA  ambazo mtandao wa dev.kisakuzi.com umezipata muda huu ni kwamba Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Dar es Salaam wamelazimika kuwatawanya vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wanaandamana kuelekea kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, anakoshikiliwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.  Taarifa zinadai kuwa …

Dk Slaa atangaza mgomo, ni kufuatia kukamatwa wabunge

*Ni kufuatia kamatakamata ya wabunge wa Chadema akiwemo Mbowe *Asema uvumilivu basi, watu waingie mtaani Na Edson Kamukara KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amewataka wafuasi wa chama hicho nchi nzima kuingia mitaani kupinga vitendo vya Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wao wakiwemo wabunge bila kufuata utaratibu. Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku mbili …

Kikombe kingine chaibuka wilayani Mpanda

Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga ULE mtindo wa baadhi ya wa kuibuka na kudai wameotesha na Mungu wakiwa usingizini waje kutoa dawa maarufu kama ‘kikombe’ kwa wagonjwa wa magonjwa sugu umeendelea na sasa mganga mwingine kaibuka wilayani Mpanda Mkoa wa Rukwa na kudai ameoteswa na Mungu kufanya kazi hiyo. Bujukano Charles Shashi (44), mkazi wa Kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Usevya ameibuka na …

Tiba ya babu yaanza kuonesha ‘madhara’

Na Maggid Mjengwa INAYODAIWA kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeanza kuonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu sasa ni mradi, na kwa kweli umeanza kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa. Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi …

Chadema kwachafuka, Mbowe, Zitto wakamatwa

Na Mwandishi Wetu KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliyekuwa akitakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mjini Arusha amekamatwa jijini Dar es Salaam.  Taarifa zilizoufikia mtandao huu zilieleza Mbowe tayari anashikiliwa na polisi wa jijini Dar es Salaam, kutekeleza amri ya mahakama ya Arusha ambapo Mbowe anakabiliwa na kesi pamoja na viongozi wengine wa …